Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi tano Prisons kapoteza moja tu

Mechi Tano Prisons Kapoteza Moja Tu.jpeg Mechi tano Prisons kapoteza moja tu

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Ligi ya NBC kurejea kutoka kwenye mapumziko kupisha Fainali za AFCON 2023, Tanzania Prisons ni miongoni mwa timu ambazo zimekusanya alama nyingi ukizitoa timu tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi [Yanga, Azam na Simba].

Timu nyingine ambazo zimekusanya alama nyingi baada ya Ligi Kuu kuendelea ni Coastal Union, Tanzania Prisons, Kagera Sugar, Ihefu na Mashujaa FC.

Tanzania Prisons imekusanya alama 10 kwenye michezo mitano iliyopita [imeshinda miechezo mitatu, imetoka sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja].

❌ Tanzania Prisons 1-2 Yanga ✅ Tanzania Prisons 3-1 Singida Fountain Gate FC ???? Tanzania Prisons 1-1 Azam FC ✅ Tanzania Prisons 2-1 Tabora United ✅ Simba 1-2 Tanzania Prisons

Katika michezo hiyo mitano, michezo mitatu ilikuwa dhidi ya timu zinazowania ubingwa msimu huu [Yanga, Azam na Simba], ni Yanga pekee ndio ilifanikiwa kuondoka na alama tatu. Azam iliondoka na alama moja, Simba imeacha alama zote tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live