Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi nne tu Ken Gold mtaipenda

Ken Gold NBC Mechi nne tu Ken Gold mtaipenda

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Pamoja na kuanza Ligi Kuu kinyonge kwa kupoteza mchezo wa kwanza, Ken Gold imesema wanaoibeza timu hiyo wasubiri baada ya michezo minne wataikubali, huku ikieleza panapovuja.

Ken Gold inashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza na katika mchezo wa kwanza dhidi ya Singida Black Stars ilipopolewa mabao 3-1 ikiwa nyumbani uwanja wa Sokoine jijini hapa na sasa inajiandaa na mechi ijayo dhidi ya Fointain Gate Septemba 11 huko Kwaraa mkoani Manyara.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fikiri Elias alisema kilichowaponza katika mchezo uliopita ni kukosa uzoefu kwa vijana wake, huku eneo la kiungo lilikosa umakini jambo ambalo benchi la ufundi linalifanyia kazi kwa kipindi hiki ili kabla ya kuwavaa Fountain Gate, kikosi kiwe fiti kutafuta matokeo.

“Najua wapo wanaoibeza, lakini nawaambia wasubiri michezo minne wataiona Ken Gold ni ya aina gani, tuliona eneo la katikati lilikosa umakini, lakini uzoefu ulitupa shinda,” alisema kocha huyo.

Elias aliongeza timu hiyo haina makosa mengi kwani eneo la ushambuliaji linao uwezo wa kumiliki mpira na kutengeneza mashambulizi, hivyo ni suala la kuongeza makali ili kupata mabao.

“Kimsingi tunaenda kusahihisha makosa ili mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate kuhakikisha tunarejesha matumaini, ari na morali ndani na nje ya uwanja,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: