Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi mbili za Yanga zapigwa kalenda

Yanga Mskms Mechi mbili za Yanga zapigwa kalenda

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeahirisha mechi mbili za timu ya Yanga SC walizopaswa kucheza Desemba 26 na 29, 2023.

Sababu ya kuahirishwa kwa mechi hizo ni kutoa fursa ya kuchezwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Zanzibar Heroes, Desemba 27, 2023.

Desemba 26, 2023, Yanga ilitarajiwa kucheza dhidi ya Kagera Sugar, mechi iliyopangwa kupigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Mchezo mwingine ulioahirishwa ni ule wa Desemba 29, 2023 dhidi ya Mashujaa ambao wenyewe ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live