Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi mbili bila bao Mapinduzi Cup 2024

Vital O X Chipukizi.jpeg Mechi mbili bila bao Mapinduzi Cup 2024

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa pili wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi kati ya Vital'O FC ya Burundi dhidi ya Chipukizi United kutoka kisiwani Pemba umemalizika katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 0-0, licha ya Vital'O FC kuwa na mchezo mzuri na kuonesha kiwango bora katika mchezo huo lakini hawakufanikiwa kupata bao lolote.

Mabadiliko ya wachezaji ya kila timu yalifanyika ili kuongeza nguvu kwenye vikosi lakini milango ilikua migumu kwa pande zote mbili.

Huu ni mchezo wa tatu kuchezwa katika Uwanja mpya wa Amaan tangu kufunguliwa lakini mpaka sasa hakuna bao lilifungwa.

Mchezo wa kwanza wa mashindano hayo ulikuwa kati ya Mlandege na Azam FC uliomalizika sare ya 0-0.

Kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa kawaida kwa timu zote mbili kwani zilishindwa kuona lango la mwenzake.

Timu hizo zilirejea kipindi cha pili kwa kuanza kushambuliana kwa mashambulizi ya hapa na pale lakini juhudi ziligonga mwamba.

Na mpaka mpira unamalizika si Azam wala Mlandege aliyeweza kuona lango la mwenzake.

leo Ijumaa Disemba 29, 2023 KVZ watashuka dimbani kuvaana na Jamhuri kutoka Pemba majira ya Saa 10:15 Alasiri, huku JKU SC watakuwa wenyeji wa Singida Fountain Gate ambae ni mshindi wa pili wa Mashindano hayo kwa mwaka 2023.

Chanzo: Mwanaspoti