Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi kumi kwa Max bila bao wala Assisti, atoa tamko

Maxi Mpiah Nzengeli Ms Mechi kumi kwa Max bila bao wala Assisti, atoa tamko

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga bado hawaelewi sana viwango vya mastaa wao akiwemo kiungo fundi Maxi Nzengeli, sasa mwenyewe amefunguka akiwaambia watulie kila kitu kitakuwa sawa ndani ya siku chache.

Nzengeli tangu ligi irejee bado hajarudisha ule ubora wake ambao ulimfanya kufunga mabao 7 akiwa pia na asisti 2 alizozitoa kabla ya ligi kusimama.

Akizungumza na Mwanaspoti Nzengeli alisema kikosi chao kipo sawa na kwamba mashabiki wao kulia kuona wanarudi kwa kasi ni ishara kwamba wanataka kitu kikubwa zaidi kwenye timu yao. Nzengeli alisema baada ya mechi mbili zilizopita mdogomdogo wameanza kufunguka na kurejea kwenye ubora wao na kwamba hilo litaendelea pia kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Mashujaa.

Kiungo huyo alisema kuwa kuanza kwao taratibu kunatokana na mazoezi mazito ambayo waliyafanya kabla ya kurejea kwa ligi ambayo yamewaongezea uimara ambayo yataendelea kuwabeba.

“Tulitoka kufanya mazoezi makali sana lakini kama mmeona kila mchezo tunabadilika, tunazidi kuwa wepesi na kila kitu kitarejea kama ambavyo mashabiki wetu wanatamani kutuona tukicheza kama ilivyokuwa nyuma,” alisema Nzengeli.

“Tuko imara sana na ndio maana tumerudi kwenye nafasi ya juu tukiongoza ligi, hesabu zetu ni kwamba sasa tuendelee kushinda na kukaa pale mpaka tutakapokabidhiwa ubingwa. Akizungumzia kufunga mabao, Nzengeli alisema lengo lake kubwa ni kuisaidia Yanga kushinda na sio kujitanguliza kutamani kufunga.

“Mimi nilishasema nilipofika hapa kitu muhimu kwangu ni kuisaidia timu kushinda mechi zake lakini kama nitafunga bao lolote itakuwa sawa, kitu napenda ni kutoa asisti ikija nafasi naona naweza kufunga nitafanya hivyo, lakini sitaki kuweka kwenye akili yangu kwamba natakiwa sana kufunga.”

Tangu michuano iliporudi, Yanga ilishinda 5-1 dhidi ya timu ya daraja la chini ya Hausung katika mechi ya Kombe la ASFC, kisha ikitoka 0-0 na Kagera Sugar ugenini kwenye Ligi Kuu kabla ya kushinda kwa tabu bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika ligi kuu.

Hata hivyo Max hanakumbukumbu ya kufunga wala ku asisti katika mechi kumi mfululizo ambazo Yanga imechezeza katika mashindano yote Ligi Kuu, Mapinduzi Cup na Kombe Azam (ASFC). Mara ya mwisho Max alifunga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba mabao mawili 64' 77' uliochezwa Novemba 5, 2023

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: