Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi EPL zitapigwa licha ya Covid-19 kuibuka

Premier League Trophy Mechi za EPL kuendelea kama ilivyopangwa

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu ambavyo vinashiriki Ligi Kuu England vimekubaliana kuendelea na ratiba za mechi za sikukuu licha ya kuibuka kwa wimbi la virusi vya Covid-19.

Vilabu hivyo 20, vimekutana Leo Jumatatu, Disemba 20, kujadili namna ya kukabiliana na hali ya Corona huku michezo sita mpaka sasa ikiwa imeahirishwa kwenye wikiendi iliyopita.

Moja ya makubaliano ni kuwa mechi za sikukuu ya kwanza za Christmas zinaweza kuendelea au kusitishwa pale panapohitajika.

Pia, wamekubalina kuwa, endapo klabu itakuwa na wachezaji 13 na golikipa italazimika kucheza mechi husika bila kuomba kuahirishwa.

Wachezaji na maofisa 42 nchini England walibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona katika wiki iliyopita ikiwa ni moja ya takwimu za juu kabisa kwa kipindi kifupi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live