Kikosi cha Yanga jana kiliibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika Dimba la Azam Complex Chamazi kwenye mchezo wa 16 bora wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).
Mabao ya Yanga yalifungwa na Bakari Mwamnyeto dakika ya 52', Clement Mzize dakika ya 70' na 88' huku akikosa penati dakika za mwisho, Stephane Aziz KI dakika ya 85 kwa mkwaju wa penati na bao la Prison lilifungwa na Jumanne Elfadhili 60 kwa mpira wa kona.
Kwenye hili bao unaweza usiyaone makosa ya defenders wa Yanga kwakuwa Yanga kaondoka na ushindi mnono na kufuzu hatua inayofuata.
Lakini, chukulia mfano Yanga haikupata nafasi ya kufunga bao na ikaruhusu bao la namna hii, hapa hakuna rangi ambayo walinzi wa Yanga wangeacha kuiona!
Wakati bao hili linafungwa ndani ya boksi la Yanga kulikua na wachezaji wa ndani 9 (na kipa Diarra wa 10) wa Yanga na wachezaji wa TZ Prisons walikua wanne tu. Lakini bado wachezaji wa Prison walifanikiwa kuugusa mpira mara mbili na kuandika bao.
Pengine mpira ungekua juu tungekuja na hoja ya kimo kama kawaida yetu ila mpira haukua juu sana na beki anaelaumiwa siku zote Dickson Job hakuwa sehemu ya mchezo.
Kipi kilitokea?
Kwanza wachezaji wa Yanga sio mashine, nao ni binadamu hivyo kisaikolojia wanayaelewa matukio yanayoendelea uwanjani
Pili, mchezo wa Mpira wa miguu huanza kuchezwa kwanza kichwani ndipo mwili unafanya kile unachotumwa kufanya. Hivyo basi, mwenye mabao mawili ya mwisho waliyofungwa Yanga kuna:-
(A) DHIDI YA AS REAL BAMAKO
Baada ya Nabi kufanya sub ya Mauya na Farid dakika ya 85 huku Yanga wakiongoza 1-0 na hakuna mashambulizi langoni kwao, wachezaji vichwani waliamini 'GAME OVER' waliamini kilichobaki ni kulinda ushindi,wakajikuta wame- switch off, dakika ya 90+1 Emile Kone, baaaaang 1-1.
(B) DHIDI YA TZ PRISON
Wachezaji wanajua wapinzani wako pungufu na tayari wanaongoza bao moja huku namba ya wachezaji wa Prison kwenye eneo lao sio kubwa sana...wakategeana dakika ya 60 Jumanne Elfadhili Chumaaaaaa 1-1.
Yanga wamefungwa magoli 5 kwenye mechi 4 za mwisho za mashindano kwa mipira iliyokufa, dhidi Prisons 1, Mazembe 1, Bamako 1 na Us Monastir 2. Ukiacha vimo vya wachezaji wao kuwa ni changamoto kubwa kwenye timu ila hata Nabi ameshindwa kufundisha jinsi gani ya kuzuia mipira ya kutenga kwa timu nzima.
MWISHO Mipira iliyokufa ni tatizo ndio maana maeneo mengine huko Duniani kuna specialist wa set pieces na wanalipwa vizuri na bado timu zinafungwa ila kwa bao la Prisons halihusiani kabisa na uwezo wa kuicheza hii mipira bali ni mentality tu.
Lakini kwenye uwanja wa mazoezi mwalimu Nabi anayo kazi kubwa ya kuhakikisha anawafundisha vizuri vijana wake namna ya kuokoa mipira ya kutenga, vinginevyo huko Kimataifa watatafuta mchawi na hawatampata.