Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mdigo apewa miwili RB Leipzig

Yussuf Poulsen Rb Leipzig Yussuf Poulsen.

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RB Leipzig imemuongeza mkataba wa miaka miwili mshambuliaji mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen.

Poulsen, ambaye anatajwa mmoja wa wachezaji bora wa muda wote wa Leipzig ambaye amekuwa na klabu hiyo tangu 2013, amesaini mkataba mpya hadi 2026.

“Kama nilivyosema hivi majuzi, bado nina hamu sana ya kuichezea RB Leipzig. Hatimaye sina jeraha tena msimu huu na ninaweza kuisaidia timu yangu uwanjani kwa muda mrefu,” alisema Poulsen baada ya kusaini mkataba wake mpya.

Mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Rouven Schröder alisema: “Hadithi ya Yussuf Poulsen hapa RB Leipzig ni ya ajabu kwa sababu ya safari yake kutoka 3. Liga hadi Ligi ya Mabingwa na kwa sababu ya muda mrefu katika klabu hii.

"Yussi ameacha alama ya kipekee kwa Leipzig kupitia mafanikio yake na haiba yake. kumbuka kwamba ana umri wa miaka 29 tu. Jinsi mashabiki wetu walivyomsherehekea uwanjani katika kuadhimisha miaka kumi ilikuwa ni dalili ya umuhimu wake kwa klabu na jiji.”

Poulsen ameichezea klabu hiyo jumla ya mechi 370 kwa miaka mingi, akifunga mabao 85 na kutoa asisti 65.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live