Wed, 6 Oct 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2021/2022 ilifungua pazia lake Septemba 27, lakini mpaka raundi ya pili ya ligi inakamilika bado ligi haikuwa na mdhamini.
Sasa hii leo Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF, linatarajiwa kusaini mkataba wa udhamini wa kuidhamini Ligi kuu Tanzania bara.
Mdhamini huyo anaetajwa ni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ingawa kiwango cha mkataba huo bado hakijawekwa wazi.
Ligi kuu kwa msimu wa 2021/2022 inashirikisha timu 16.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live