Kuna wakati tunahitaji kukaa kimya ili kuficha uchi wa akili zetu kwenye jamii ya watu wenye uelewa!
Kwanini...?
Mtu anaejinasibu anajua kila kitu hasa kuhusu football na history yake kwenye nchi hii... anaposema Timu fulani haijafika Nusu fainali au fainali ya Kombe la CAF kwa kuweka ushahidi huu wa hii tweet maana yake hana anachokijua kwenye football
Yes, Ni bora ukakaa kimya pengine tutajua unajua kumbe hujui..!
Tweet ya CAF inaelezea mashindano ya CAFCL haimaanishi mashindano yote!
Yaani ni sawa na timu kama Mtibwa Sugar ambayo imewahi kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu ikifika hatua ya fainali ya FA kama haijawahi kutwaa FA tutasema Mtibwa inatafuta rekodi ya kutwaa Kombe la FA kwa mara ya kwanza!... HAIMAANISHI HAWAJAWAHI KUTWAA LIGI KUU AU LIGI NYINGINE INAYOSIMAMIWA NA TFF
Nyie mnazungumzia football ya wapi nyie...?
Mfano, Celtic ikifika fainali ya Europa itakua inatafuta rekodi ya kutwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza lakini Celtic hao hao walishatwaa UEFA mwaka 1967 baada ya kumfunga Inter Milan 2-1 pale Estádio Nacional, Lisbon.
Mfano mwingine rahisi, Real Madrid ana mataji 14 ya UCL lakini haijawahi kutwaa UEFA Europa Conference League, Ikifika fainali tutaandika kwamba Real Madrid inatafuta rekodi ya kutwaa Conference League kwa mara ya kwanza, haimaanishi Real Madrid haijawahi kutwaa Kombe linalosimamiwa na UEFA.
Rs Berkane ana mataji mawili ya CAFCC na moja la CAF SUPER CUP...Lakini hajawahi kuingia robo fainali ya ligi ya Mabingwa (CAFCL) Maana yake siku akifika group stage tutasema anatafuta rekodi ya kuingia hatua ya robo fainali ya CAFCL kwa mara ya kwanza japo alishabeba mataji mengine ya yanayosimamiwa na CAF.
Bahati mbaya sana mtu anapotosha umma akidhani wote hawajui ispokuwa yeye na ndo mnaemsikiliza!!
Kuhusu Simba kufika fainali hayo muulizeni yeye si alikua huko huko .
Mpaka sasa bado hatuajua ukweli ni upi, hebu na wewe msomaji wa Tanzaniaweb tuachie commment yako katika hili