Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mdau: Tatizo la Azam liko hapa, wala si kocha

Azam FC Kuwasilini.png Mdau: Tatizo la Azam liko hapa, wala si kocha

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam Fc ni Timu ambayo machoni na moyoni imekamilika kwa Kila kitu kwa Maana ya Wachezaji na Miundombinu ambayo inachagizwa na Uwekezaji Mzuri wa Wamiliki unaohitaji matokeo kwa kuweka Technical Bench lenye kila aina ya hitaji lakini wamesahau kitu muhimu sana Katika Soka la Kisasa nacho ni FOOTBALL CLUB MANAGEMENT SYSTEM.

Kwa muda sasa Azam Fc Imeweza kupitia katika vipindi tofauti Tofauti sana na kupata Aidha wachezaji au Technical Bench zuri tu na lenye uzoefu ila wanashindwa kupata Matokeo kulingana na mahitaji hapa ndio unapoona Kuna Tatizo zaidi ya yanayoonekana machoni.

Tukirudi Nyuma Utaweza kuona Kocha kama Stewart Hall ameweza kufundisha kwa vipindi Vitatu Tofauti 2010, 2012 na 2016 pia Kocha Aristica Cioaba nae amefundisha vipindi Viwili 2017 na 2020 hawa wote ukiangalia kwa makini wameweza kurudi kutokana waliondoka sio kwa wao kuwa wabavu bali ni kukitetea kwa Management tu.

Kocha wa sasahivi DENIS LAVAGNE ni moja wa Makocha wazoefu wabobevu na wenye hadhi ya juu katika Soka la Africa amefeli mpaka sasa ukiangalia lazima utaona moja ya matatizo ni kutokana na Management.

Football Club Management System ndio Tatizo Kuu kwa Azam Fc ambalo likitibiwa hili haya mengine ya Technical Bench yatajipanga vizuri bila wasiwasi na hili haliwezi kuongelewa vizuri na watu wengi ndani ya Azam kwa maana wanaoneana Aibu, kuogopana na Kusitiriana ila wakati ukifika likavukwa hili tutaona Azam fc iliyokamilika katika Idara zote.

Hatuwezi Kuendesha Mpira kwa Maagizo, Kwa kusubiria nani atasema nini au kuendana na upepo ulivyo wala Kuendesha mpira kwa kutegemea kazi zingine mara ukifanya kosa huku unapelekwa huku mfumo huu haupo katika Soka la Kisasa.

Club lazima Iwe na Watu waliokuwa Full Responsibility za kila siku katika Utendaji na wenye uwezo wa kusema hiki hapana sio Ndio Mzee ambao watawajibika katika chombo cha Juu cha Uangalizi.

Katika Tanzania tuna Imani na Azam Fc na tunajivunia katika Uwekezaji wake ila Tunaangushwa hakuna Management bali kuna Usimamizi wa Timu ni muda sasa wa kupata Watu Tofauti Tofauti wanaojua soka la Africa ndani na nje ya Tanzania waende Kutenda haki kwa Soka pale Chamazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live