Mon, 24 Jan 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
KLABU ya FC Porto ya Ureno kuna uwezekano ikaachana na Beki wake Chancel Mbemba, Raia wa Congo DR baada ya kugundua kuwa Mchezaji huyo amedanganya umri wake.
Mbemba inaelezwa kuwa ana tarehe 4 tofauti za kuzaliwa zilizopo katika vyeti vyake vya kuzaliwa vinne tofautitofauti.
Mbemba ambaye kwa sasa anadai kuwa na umri wa miaka 27 inatajwa kuwa anaweza kuwa mkubwa kwa miaka mitano zaidi ( 32), Porto wanataka kumuacha mwisho wa msimu AC Milan na vilabu kadhaa Ulaya vilikuwa vikimuhitaji lakini tuhuma za kudanganya umri zimefanya wasite kufanya hivyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live