Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mcolombia wa Azam FC aikataa jezi

Franklin Navarro Azam Mcolombia wa Azam FC aikataa jezi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Franklin Jesus Navarro, nyota mpya wa Azam FC kutoka Colombia, ameikataa namba ya jezi aliyoandaliwa na klabu hiyo.

Navarro ambaye kwao alikuwa akivaa jezi namba 10, aliandaliwa jezi namba 13 ambayo alitambulishwa nayo na kuvaa siku alipocheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Chipukizi.

Akizungumza baada ya mazoezi ya Januari 6 kuelekea mechi ya robo fainali dhidi ya Singida Fountain Gate, Navarro alisema ameomba abadilishiwe namba ya jezi kwa sababu namba 13 siyo ya bahati.

“Niliwahi kuvaa namba 13 na sikuwa na wakati mzuri hadi nikaamua kubadilisha.”

Navarro alivaa jezi namba 13 msimu wa 2018/19 akiwa na Leonnes FC ya kwao Colombia.

Katika historia yake ya soka, Navarro amevaa jezi za namba tofauti kama ifuatavyo.

2018/19

Leonnes FC - namba 13

2019/20

Llaaneros FC - namba 10

2020/21

CD Real Cartagena - 30

2021/22

Carabobo FC - 25

2022/23

Cortulua - 10

2023/24

Azam FC - 13

Pumzi ya Moto ikamtafuta Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabith Zakaria maarufu kama Zaka Zakazi, kutaka kujua kama klabu imeshalifanyia kazi ombi la mchezaji wao huyo mpya.

“Ni kweli kwamba Don Navarro ameomba kubadilishiwa namba ya jezi, na klabu haina tatizo na hilo,” alisema Zaka.

Alipoulizwa kuhusu namba mpya, Zaka alisema watampa namba 8 ambayo tangu aondoke Ibrahim Ajibu, Januari 2023 imekosa mtu.

“Tunaheshimu maombi yake na tayari tumeyafanyia kazi kwa kumpatia namba 8 ambayo ameridhia.

Tulimpa namba 13 kwa sababu ipo katika orodha ya jezi ambazohuko nyuma alivaa katika jezi ambazo zilizo wazi kwetu,” aliongeza Zaka.

NAMBA YA MIKOSI

Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti ya Stress Management Center and Phobia Institute ya Asheville, North Carolina, Marekani, zaidi ya asilimia 80 ya majengo marefu nchini humo hayana ghorofa ya 13, na mahoteli mengi, mahospitali na hata viwanja vya ndege hukwepa kutumia namba 13 kwenye vyumba na mageti.

Ubaya wa namba 13 unatokana na uzuri wa namba 12.

Kwa tamaduni za Afrika Magharibi namba 12 inahusishwa bahati na ukamilifu, ndio maana kuna siku 12 za Krismasi. Kuna miezi 12 katika mwaka na kuna alama za unajimu yaani utabiri wa nyota.

Siku yenye saa 24 imegawanywa mara mbili katika vipindi vya saa 12 kila kimoja.

Kuna miungu 12 wa Olympus (Kigiriki) na kuna makabila 12 ya Israel.

Kwa kifupi namba 12 ni ya baraka zote katika imani hizo. Namba inayofuata baada ya hapo ni 13 ambayo inakuja ikikuta baraka na bahati zote zimeshachukuliwa na namba 12 ikaishia kuchukua mikosi tu.

Hii ni sawa na hadithi ya Biblia ya watoto mapacha wa Nabii Isaka; Esau (Kulwa) na Yakobo (Dotto).

Esau alipoondoka, Yakobo akapata baraka na bahati zote, Essau aliporudi akachukua vilivyobaki ambavyo vilikuwa mikosi na bahati mbaya.

Kwa hiyo namba 13 imechukua mabaya yote, mikosi yote na bahati mbaya zote.

Mfalme wa zamani wa Mesopotamia, Hammurabi, aliiondoa sheria namba 13 katika sheria zake maarufu zinazoitwa Code of Hammurabi yaani sheria za Hammurabi.

Hii ni moja ya ushahidi mkuu wanaoutumia watu wote wanaoihofia namba 13 kuwa ya mikosi.

Hamuurabi aliiongoza Mesopotamia kati ya mwaka 1792 hadi 1750 kabla ya kuzaliwa Kristu. Mesopotamia kwa sasa ndio nchi ya Iraq.

Sheria za Hammurabi ndio sheria za kwanza kabisa kuandikwa kwa ukamilifu wa hali ya juu duniani katika historia ya sheria.

Katika mwendelezo wa ubaya wa namba 13, Magharibi kuna madharia inaitwa Friday the 13th yaani Ijumaa ya 13.

Nadharia hii inatokana na simulizi ya Kibiblia ya kwenye karamu ya mwisho ya Alhamisi Kuu.

Watu 13 walihudhuria karamu hiyo, akiwemo Yesu na mitume wake 12 mmojawao akiwa Yuda ambaye baadaye alimsaliti.

Siku iliyofuata ilikuwa Ijumaa Kuu, siku ambayo inaelezwa kwa mujibu wa Biblia kwamba ndio Yesu alisulubiwa.

Mpangilio wao mezani kwenye ile karamu ukasababisha watu waogope kukaa 13 wakati wa kula.

Franklin Navarro anatokea Colombia, nchi ya Kilatini yenye utamaduni wa Kimagharibi.

Mambo yote hata wanayajua na kuyafuata na kuyaamini. Inawezekana Navarro jezi namba 13 aliyoitumia mwaka 2018, kuna mambo yalimtokea na kuogopa moja kwa moja.

WACHEZAJI NA NAMBA

Mikasa ya namba za jezi kwa wachezaji imekuwa ikitokea kwa miaka mingi, kwa vyanzo tofauti.

Wachezaji mbalimbali wamekuwa wakivaa jezi za namba kutokana na imani, historia au siri fulani.

KOULIBALLY 26

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Kalidou Koulibally, amekuwa akivaa jezi namba 26 katika klabu zote anazozichezea.

Hii ni kwa sababu ya kufurahia maisha yake ya uhusiano na mpenzi wake, Charline Oudenot.

Koulibaly na mpenzi wake wanafanana siku zao za kuzaliwa, japokuwa ni miaka tofauti.

Wote wamezaliwa tarehe 20 mwezi wa sita, ndio maana ya 26 yaani 20+6.

Akiwa Napoli, aliivaa namba hii kwa misimu minane, tangu alipojiunga nayo mwaka 2014 hadi alipoondoka 2022.

Na hata alipohamia Chelsea aliikuta namba hiyo haitumiki kwa heshima ya nahodha John Terry.

Koulibally akamuomba Terry amruhusu kuitumia. Terry akakubali na Koulibally akaivaa.

PHILI FODEN NAMBA 47

Nyota wa Manchester City na Timu ya Taifa ya England, Phil Foden yeye anavaa jezi namba 47 klabuni kwake.

Foden aliichagua namba hii kama kumbukumbu kwa bibi yake ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 47.

BRUNO GUIMERAS NAMBA 39

Nyota huyu wa Newcastle United na Timu ya Taifa ya Brazil, anavaa jezi namba 39 klabuni kwake kama heshima kwa baba yake mzazi ambaye alikuwa dereva wa teksi mwenye namba hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti