Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mcolombia atwishwa zigo la lawama Azam FC

Jhonier Alfonso Blanco Mshambuliaji mpya wa Azam FC Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Azam FC Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco amepewa mikoba ya kikiongoza kikosi hicho katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho ambacho kilimsajili kutoka Klabu ya Rionegro Aguilas ya kwao Colombia baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika timu ya Fortaleza CEIF aliypkuwa anaichezea kwa mkopo.

Msimu uliopita nyota huyo aliibuka mfungaji bora akiwa na timu hiyo ya Fortaleza CEIF inayoshiri Ligi Daraja la Kwanza Colombia, (Categoría Primera), baada ya kufunga jumla ya mabao 13.

Kikosi kamili cha Azam katika mchezo huo, kinaundwa na Mohamed Mustafa, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Yeison Fuentes, Yannick Bangala, Adolf Mtasigwa, Franck Tiesse, James Akaminko, Jhonier Blanco, Feisal Salum 'Fei Toto' na Gibril Sillah.

Wachezaji wa akiba ni Zuberi Foba, Abdallah Kheri 'Sebo', Nathaniel Chilambo, Cheikh Sidibe, Nassor Saadun, Adam Adam, Idd Suleiman 'Nado', Yoro Mamadou Diaby, Ever Meza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live