Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Mashimo: Yanga sio bingwa msimu huu

IMG 5363 Mashimo.jpeg Mch. Mashimo: Yanga sio bingwa msimu huu

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Mashimo amefunguka kuwa Klabu ya Yanga haitotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kutokana na kukiuka Sauti ya Mungu.

Mashimo amesema Yanga wameshindwa kumpa asilimia 10 ya fedha walizizipata kwenye goli la mama wakati wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022/23 ambapo Yanga ilifika hatua ya fainali.

Aidha, Mchungaji Mashimo ameenda mbali zaidi akidai kuwa iwapo Yanga SC watampa asilimia 10 ya fedha walizozipata kutoka kwa Rais Samia, basi mambo yatabadilika.

"Bwana asifiwe, timu iitwayo Yanga haitotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu kwa kukiuka sauti ya Mungu kwa kutonipa asilimia kumi ya fedha walizipata kwenye magoli ya mama kwenye mashindano ya Afrika Msimu uliopita, na kama uongozi wa Yanga utaamua kunilipa hizo asilimia 10 hata leo mambo yatabadilika," amesema Mchungaji Mashimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live