Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchumba wa Greenwood ahudhuria utambulisho wake Hispania (+Video)

Mason Greenwood Wife.jpeg Mpenzi wa Mason Greenwood Harriet Robson

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Juzi kwenye Utambulisho wa Wachezaji wa klabu ya Getafe kwenye dimba la Coliseum Alfonso perez, mpenzi wa Mason Greenwood Harriet Robson alikuwa ni sehemu ya watazamaji wa mazoezi hayo.

Mrembo Harriet alikuwepo uwanjani hapo kumsapoti Greenwood ambaye ameanza maisha mapya ya soka baada ya kukumbwa na maswahibu kadhaa ambayo yalimfanya awe nje ya uwanja kwa muda.

Harriet aliweka picha ya jezi ya mtoto yenye namba 12 ambayo ndio namba ya Mpenzi wake kunako klabu hiyo ikiwa na jina DADDY mgongoni.

wawili hao walipata mtoto wao wa kwanza mwezi julai mwaka huu.

Mason alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ya unyanyasaji wa kijinsia,Ubakaji ambayo Harrieth ndiye alisababisha kwa kumfungulia mashtaka hayo mpenzi wake lakini baadae Mason akaonekana hana hatia baada ya uchunguzi.

Mason amemsamehe mrembo huyo na maisha yanaendelea kama kawaida.

View this post on Instagram

A post shared by Van_for_sports_ (@van_for_sports_)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live