Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchongo wa Arteta ndo huu

Arteta Mikelll Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amevutiwa na straika wa Barcelona, Ferran Torres na anataka kujaribu bahati ya kumnasa dirisha dogo la Januari.

Arsenal inataka kufanya usajili wa straika mwingine kama mbadala wa Gabriel Jesus ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumia kwenye mechi ya raundi 16 bora ya michuano ya Kombe la Dunia, Brazil ilipocheza dhidi ya Cameroon.

Arteta alikuwa anamfukuzia fowadi huyo wa zamani wa Manchester City kwa muda mrefu kabla ya Torres hajajiunga na Barcelona.

Kwa mujibu wa ripoti Barcelona ipo tayari kumuachia Torres baada ya kocha Xavi Hernandez kutoridhishwa na uwekezaji wa klabu hiyo uliogharimu Pauni 46.3 milioni hadi kumnasa akitokea Man City. Vilevile timu nyingine zimeendelea kufuatilia hatima ya Torres ikiwemo AC Milan na Tottenham Hotspur. Lakini Arteta anataka kupindua meza na kuzipiku.

Kwa sasa Torres yupo mapumziko baada ya Hispania kutolewa Kombe la Dunia.

Chanzo: Mwanaspoti