Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchongo wa Arsenal bila Jesus

B9E2CA67 2402 480F 8E45 D2F111407866.jpeg Gabriel Jesus

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal inarudi leo kuendelea na mbio za kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham baada ya michuano ya Kombe la Dunia kule Qatar ambayo ilimalizika kwa Argentina kutwaa bingwa.

Vinara hao wa ligi wanawakaribisha West Ham huku Mikel Arteta akiwa na matumaini ya kutoka na matokeo mazuri ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo.

Hata hivyo, Arsenal itakuwa bila ya straika tegemeo Gabriel Jesus baada ya kuumia goti na kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita. Fowadi huyo aliumia kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon.

Arteta amekuna kichwa ni straika gani ambaye anayeweza kuziba pengo la Mbrazil huyo na Eddie Nketiah ndiye anayepewa nafasi kubwa baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mechi za kirafiki hivi karibuni.

Sasa kikosi cha Arsenal kitabadilika na hakitakuwa kama kile kilichocheza na kupata ushindi dhidi ya Wolves kabla ya mapumziko kupisha Kombe la Dunia.

Pamoja na Jesus, Arsenal ina wachezaji majeruhi akiwamo Reiss Nelson aliyeumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Juventus, na bado haijafahamika atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.

Emile Smith Rowe huenda akarejea leo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na huenda akaanzia benchini. Licha ya Oleksandr Zinchenko kutojumuishwa kwenye mechi tatu za kirafiki mfululizo zilizopita, beki huyo huenda akaanza leo dhidi ya West Ham.

Lakini Kieran Tierney huenda asipangwe mbele ya Zinchenko kwani imeelezwa Tierney bado anasumbuliwa na maumivu ya shingo.

Kutokuwapo kwa Jesus, kocha Arteta anaweza akachezesha mfumo wa 4-2-3-1, Gabriel Martinelli anaweza kuongoza mashambulizi na nyuma yake watawapo Bukayo Saka, Odegaard na Smith Rowe. Arteta hana uhakika endapo atasajili straika mwingine dirisha la Januari.

Chanzo: Mwanaspoti