Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezo wa Liverpool vs Leeds waota mbawa

Anfield Mchezo wa Liverpool na Leeds wapigwa kalenda

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Ligi Kuu England umeahirisha mchezo baina ya wenyeji Liverpool na Leeds United pamoja na mchezo wa Wolves na Watford kutokana na hofu na kuibuka kwa wimbi la nne la virusi vya Corona.

Timu zote mbili zilikuwa zina ratiba ya kushuka dimbani Disemba 26 Jumapili lakini kutokana na maombi ambayo yameifikia meza ya Epl, imeamua kuziotesha mbawa mechi hizo.

Taarifa ya Ligi ilisema Leeds United haitaweza kucheza baada ya wachezaji wake kukutwa na dalili za Uviko-19 wakati wachezaji wengine wakiwa na majeruhi na wagonjwa.

Kocha wa Everton Rafael Benitez alisema anashangaa mchezo wake na Burnley uko pale pale licha ya kuathirika pia na janga hilo kwani mchezo wa mwisho kucheza ulikuwa baina yao na Chelsea katika sare ya 1-1 kabla ya mtanange wa Leicester City kupigwa kalenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live