Kiungo wa Simba, Clatous Chama anaimani mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union utakuwa sehemu ya kusahihisha makosa yao kuelekea mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Chama ambaye ameisawazishia Simba na kutoka uwanjani kwa matokeo ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos katika mchezo iliopigwa juzi uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia.
Chama alisema kabla ya kuwaza mechi ya marudiano hapo kati kuna mchezo wa ligi , wanaporejea wataanza maandalizi ya mechi hiyo ya ligi kuu dhidi ya Coastal kabla ya kurudiana na Power Dynamos.
“Hapa kati kuna mechi ya ligi, akili na nguvu tunaelekeza kwenye mchezo huo, tukimaliza mechi hiyo tunaingia katika maandalizi ya kupambana kwa ajili ya kusaka ushundi wa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika .
“Ninaimani Dar es Salaam tutapambana zaidi , katika mpira chochote kinaweza kutokea sare ilikuwa sio lengo letu, tunaenda kupambana katkka mechi ya marudiano, ” alisema Chama.
Aliongeza kuwa mechi ilikuwa ngumu wachezaji walipambana kuhakikisha wanasawazisha licha ya Power Dynamos walibadilika tofauti na waluvyocheza awali.
Chama alisema baada ya kufungwa bao la kwanza walifanikiwa kujiandaa kiakili na kimwili kwa kupeana ishara ya kupambana hadi hatua ya mwisho kusawazisha mabao hali iliyotokea kwenye mechi hiyo.
“Muhimu sana kucheza kwa mahitaji ya timu, kocha na kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wamekuwa wakiwa pamoja na sisi katika kila hatua , hatuwezi kuwaambia kwa maneno bali kuhakikisha tunawafurahisha kwa matokeo mazuri uwanjani,” alisema Chama.
Simba imerejea Dar es Salaam na inaingia kambini kwa amaandalizi ya michezo iliyopo mbele yao ikiwemo huo wa marudiano utakaopigwa Oktoba mosi , mwaka huu.