Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji wa timu ya Al-Ittihad acharazwa viboko na shabiki Saudia

Mchezaji Wa Timu Ya Al Ittihad Acharazwa Viboko Na Shabiki Saudia Mchezaji wa timu ya Al-Ittihad acharazwa viboko na shabiki Saudia

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Shirikisho la Soka la Saudi Arabia litakagua upya kanuni za maadili ya mashabiki baada ya shabiki mmoja kuonekana akimchapa viboko mchezaji wa Al-Ittihad.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mechi baada ya Al-Ittihad kufungwa na Al-Hilal katika michuano ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi.

Picha zinaonyesha mshambuliaji wa Al-Ittihad, Abderrazak Hamdallah akimrushia maji shabiki, ambaye kisha anampiga mchezaji huyo mara mbili kwa kile kinachoonekana kama mjeledi.

SAFF ilisema "imeshtushwa na matukio ya aibu".

Hamdallah wa Morocco aliifungia timu yake ilipopoteza kwa mabao 4-1.

"Kandanda nchini Saudi Arabia ni mchezo wa familia na, tunashukuru, machafuko ya mashabiki ni nadra sana," SAFF ilisema.

"Ndio maana vitendo vya shabiki ''huyu'' vinaenda kinyume na yote ambayo soka la Saudia linawakilisha na tunalaani vikali tukio hilo."Kutakuwa na ukaguzi wa kina wa maadili ya mashabiki. Ukaguzi huo utahakikisha sheria na kanuni zilizoboreshwa zinawekwa ili kutoa adhabu kwa haraka ili kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya."

Chanzo: Bbc