China imethibitisha kumkamata Mwanasoka kutoka Korea ya Kusini Son Jun-ho (31) kuhusiana na kesi ya rushwa.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Jun-ho ambaye anaichezea Super League ya China pamoja na timu ya taifa ya Korea Kusini anashikiliwa na polisi katika jimbo la Lianoning.
Kukamatwa kwa kiungo huyo katika uwanja wa ndege huko Shanghai ijumaa iliyopita kunakuja wakati soka la China likiwa limezungukwa na tuhuma za rushwa na upangwaji wa mechi kinyume na sheria.
Takribani wachezaji wanne wa soka wamekamatwa nchini China katika miezi mitatu iliyopita kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na soka.