Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji atupwa jela mwaka mmoja

Akinkunmi Amoo.jpeg Akinkunmi Amoo

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasoka kutokea Nigeria, Akinkunmi Amoo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa unyanyasaji wa kijinsia wa Wanawake watatu nchini Denmark.

Mchezaji nyota wa zamani wa Golden Eaglets, amepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingono na Mahakama ya Wilaya nchini Denmark.

Nyota huyo wa FC Copenhagen mwenye umri wa miaka 20, ambaye alishtakiwa kwa kuwalawiti Wanawake watatu, alihukumiwa siku ya Ijumaa, Juni 23, 2023.

Mahakama iliripotiwa kumpiga marufuku ya miaka sita ya kuingia Denmark. Inasemekana mchezaji huyo amekata rufaa dhidi ya uamuzi huo, ingawa haijajulikana ni lini rufaa hiyo itapelekwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live