Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji apigwa Pingu kwa kumpiga mwamuzi Rwanda

InShot 20240404 1002015302 732x439 Mchezaji apigwa Pingu kwa kumpiga mwamuzi Rwanda

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo kati ya timu ya Fatima FC na Gatsibo wa hatua ya robo fainali ya Peace Cup kwa upande wa Wanawake nchini Rwanda umekumbwa na vurugu huku mchezaji akipigwa pingu na Mwamuzi kujeruhuhiwa.

Vurugu zilizuka dakika ya 87 ya kipindi cha pili baada ya Nahodha wa klabu ya Fatima FC, Usanase Djamila kupewa kadi nyekundu kwa kuunawa mpira ndani ya 18 na kukataa kukubaliana na maamuzi ya Mwamuzi na kumrushia ngumi.

Kadi hiyo nyekundu ilisababisha benchi zima la Fatima kuingia uwanjani na Polisi kuingilia kati na kumkamata mchezaji wa Fatima FC,Uwiragiye Chantal kwa kumjeruhi mwamuzi.

Shirikisho la soka nchini Rwanda kupitia kwa Katibu wake Mkuu Adolphe Kalisa limefahamisha kuwa limesubiri ripoti kutoka kwa Kamishna wa mchezo kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live