Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji akamatwa kwa kugusia vita ya Israeli

Mchezaji Akamatwa.jpeg Mchezaji akamatwa kwa kugusia vita ya Israeli

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji Sagiv Jehezkel, raia wa Israel aliyeonyesha ujumbe unaorejelea vita vya Israel na Hamas wakati wa mechi kati ya timu yake ya Antalyaspor ya Uturuki amekamatwa.

Kwa mujibu wa ripoti katika vyombo vya habari vya Uturuki, Waziri wa Sheria wa nchini Uturuki, Yilmaz Tunç ameagiza kufanyika uchunguzi dhidi ya Jehezkel kuhusu tukio hilo kwa tuhuma za "uchochezi wa chuki".

Uchunguzi huo unakuja huku klabu ya Antalyaspor ikiwa imesimamisha mchezaji huyo kutoka na ujumbe aliouonyesha.

Jehezkel alionyesha ujumbe aliokuwa ameandika kwenye bendeji kwenye mkono wake wa kushoto ukisomeka “siku 100. 07/10” akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake bao dakika ya 68 dhidi ya Trabsonspor.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1 jana Jumapili, Januari 14, mwaka huu katika Ligi Kuu ya Uturuki.

Ujumbe huo ulikuwa ukirejelea shambulio la Hamas dhidi ya Israel Oktoba 7, 2023 na idadi ya siku ambazo zaidi ya mateka 130 wa Israel wameshikiliwa huko Gaza.

Shambulio lisababisha Israel kulipa kisasi na mpaka sasa jeshi la nchi hiyo limeua watu zaidi ya 23,000 huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live