Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji aitumikie timu sio timu imtumikie mchezaji

Camavinga X Novatus Mchezaji aitumikie timu sio timu imtumikie mchezaji

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpira wa kisasa ‘modern football’ inamlazimisha mchezaji kuitumikia timu na sio timu kumtumikia mchezaji, mchezaji yupo uwanjani kwa ajili ya kuisaidia timu sio kujinufaisha mwenyewe. Zamani ilikuwa mchezaji anaamua kuwa man of the show lakini sasa hivi kutokana na matumizi ya muda na nafasi hakuna tena mambo hayo.

Ndio maana siku hizi utaona kocha anatumia mchezaji kwenye eneo tofauti na watu wengi walipozoea kumuona, mchezaji huyohuyo kwenye timu ya kocha mwingine hapati nafasi licha ya ubora alionao.

Mpira wa kileo Kocha ndio anaamua timu ichezaje kulingana na majukumu anayowapa wachezaji uwanjani, kwa hiyo mchezaji ambaye hatekelezi majukumu ipasavyo hawezi kupata nafasi kwenye kikosi hata kama ni bora kwa kiasi gani.

Ndio hapo ambapo makocha wengi wanaingia kwenye lawama za madhabiki kwa nini mchezaji fulani hachezi wakati ana uwezo mkubwa. Makocha wengi sasa hivi wanaangalia uwiano wa timu wakati ikiwa na mpira, ikiwa haina mpira, namna gani inazuia na namna gani inashambulia.

Ndio maana kuna mchezaji anaweza kutumiwa na Kocha kama beki wa kushoto, beki wa kati au kiungo na timu ikanufaika na uwepo wake uwanjani.

Wachezaji wengi wanaonufaika na mifumo ya soka la kisasa ni wale ambao wamekulia kwenye academy kwa sababu wanafundishwa na wanajua kila nafasi na majukumu yake uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live