Klabu ya Inter Milan juzi ilipokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Fiorentina katika dimba la San Siro katika mchezo wa Serie A huku tukio la mchezaji wa Fiorentina kucheza na akili ya Mwamuzi ili mwenzake afuturu likiibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki.
Wakati wa mechi hiyo, mlinzi wa Fiorentina, Luca Ranieri raia wa Italia, alidanganya kuumia ili kumwezesha mchezaji mwenzake Sofyan Amrabat raia wa Morocco kufuturu, jambo ambalo liliibua hisia tofauti kutoka kwa wafuasi wa mchezo wa soka.
Ligi kuu ya Serie A kama ilivyo kwa Ligi zingine 5 bora za Ulaya (England, Ufaransa, Uhispania na Ujerumani na Italia ) isipokuwa Ligi kuu England hazijapitisha sheria ya kusimamisha mchezo ili wachezaji wafuturu. Ni Ligi kuu England pekee ndio imepitisha sheria hiyo.