Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji aachana na mkewe baada ya kugundua analea watoto sio wake

Mchezaji Aachana Na Mkewe Baada Ya Kugundua Analea Watoto Sio Wake Mchezaji aachana na mkewe baada ya kugundua analea watoto sio wake

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na ‘klabu’ ya Chelsea Geremi Njitap ameripotiwa kuachana na mkewe baada ya kugundua kuwa watoto mapacha aliowalea siyo wake

Taarifa hizo zinakuja baada ya Geremi (45) kufanya Vipimo vya Vinasaba (DNA) na kuonesha kuwa Mapacha hao ambao mkewe aitwaye Toukam Fotso Laure Verline alimuaminisha ni wake, sio wake Kibaiolojia.

Kwa mujibu wa nyaraka zinazosambaa mitandaoni Geremi amefungua kesi mahakamani akilalamika kukosewa heshima na mkewe ambaye alikuwa akimtolea lugha za dharau mbele ya watoto hao.

Geremi Njitap aliwahi kukipiga katika ‘timu’ kama Real Madrid, Middlesbrough na Newcastle United akiwa kama beki wa kulia pamoja na kiungo mkabaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live