Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Ligi Kuu atiwa nguvuni kwa tuhuma za kubaka

Yenyewe 1 Mchezaji Ligi Kuu atiwa nguvuni kwa tuhuma za kubaka

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ametiwa nguvuni na maafisa wa Polisi nchini humo kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ubakaji.

Polisi hao wa Metropolitan wamesema kuwa taarifa za kubakwa kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 20 ziliwasilishwa kituoni kwao. Aidha wameendelea kubainisha kuwa tukio hilo limeripotiwa kutokea mwezi Juni 2020.

Katika taarifa iliyotolewa na Metropolitan ilibainisha kuwa mtuhumiwa alikamatwa katika anwani ya mji wa Barnet ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahabusu ambapo bado yupo hadi sasa. Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa.

Kwa miaka ya hivi karibuni matukio ya ubakaji yameshamiri sana miongoni mwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Uingereza likiwemo sakata la mchezaji wa zamani wa Manchester City na Sunderland pamoja na Timu ya Taifa ya Uingereza Adam Johnson lakini pia mchezaji wa Manchester City na Timu ya Taifa ya Ufaransa Benjamin Mendy ambaye hadi sasa yupo kizuizini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live