Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Kaizer Chiefs afariki Dunia

Steven Ncanana Steven Ncanana

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Timu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini, Steven Ncanana ameaga dunia wikendi iliyopita akiwa na umri wa miaka 36.

Habari hizo za kusikitisha zilithibitishwa na kaka yake, Leonard, ambaye alisema Ncanana alifariki dunia Jumapili asubuhi baada ya kufikishwa hospitalini hapo siku chache zilizopita kwa ajili ya kupatiwa huduma .

"Ndiyo, hayuko tena," Leonard Ncanana aliambia iDiski Times.

"Alikuwa mgonjwa kwa muda. Hii ilianza siku chache zilizopita na tulipigia simu ambulance ili kumchukua ambayo ilikuja akiwa na hali mbaya.

“Siku ya Alhamisi, nilipiga simu hospitali kuomba kuonana naye asubuhi, jambo ambalo nilifanya. Kisha nilipokuwa nikienda kwenye mazoezi, nilipokea simu siku ya Jumapili kwamba niende hospitali na nilipo enda nikaambiwa hayupo tena.”

Ncanana alijiunga na Kaizer msimu wa mwaka 2010/11 chini ya kocha Vladimir Vermezovic pamoja na Sthembiso Ngcobo, Dominic Mateba, Stanton Lewis na Siyabulela Songwiqi.

Katika msimu wake wa kwanza, Ncanana alishinda taji lake la kwanza akiwa na kaizer baada ya kuwafunga wapinzani wa Orlando Pirates kwa bao 3-0 katika Dimba la FNB Stadium wakati wa fainali ya Telkom.

Msimu wa 2015/16, Ncanana alirejea Thanda Royal Zulu ambako Kaizer Chiefs walimnunua hapo awali ambako aliwatumikia kabla ya kutimkia AmaZulu msimu wa 2017/18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live