Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Geita Gold atekwa na watu wasiojulikana

Zdc Geofrey Mchezaji Geita Gold atekwa na watu wasiojulikana

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya soka ya Geita Gold unalaani vikali tukio la kutekwa na kushambuliwa kwa mchezaji wao Geofrey Rafael maarufu “Geofrey Muha” tukio lililotokea usiku wa kuammkia Februari 19, 2024.

Taarifa ya Geita imeeleza kuwa Geofrey alipatwa na madhira hayo ya kushambuliwa na watu asiowafahamu waliokuwa na vitu vyenye ncha kali na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kabla ya wasamaria kumpa msaada.

Imeelezwa kuwa Geofrey yupo Hospitali chini ya uangalizi maalumu wa madaktari akipatiwa matibabu ili kurejesha afua ya mwili wake.

Aidha Jeshi la polisi tayari limechukua hatua na linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live