Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Díaz awaomba watekaji nyara wa baba yake wamuachilie

Mchezaji Mchezaji Díaz awaomba watekaji nyara wa baba yake wamuachilie

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mchezaji kandanda wa Liverpool mzaliwa wa Colombia, Luis Díaz amewasihi watekaji nyara wa baba yake wamuachilie mara moja na "kumaliza kusubiri huku kwa maumivu".

Wazazi wote wawili wa Díaz walikamatwa wakiwa wamenyooshewa bunduki katika mji aliozaliwa wa Barrancas na waasi wa mrengo wa kushoto wa Jeshi la Ukombozi la Kitaifa (ELN) tarehe 28 Oktoba.

Wakati mama yake alipatikana, baba yake bado hajaachiliwa .

Díaz alifunga bao dhidi ya Luton siku ya Jumapili, akiinua jezi yake kufichua maneno kwa Kihispania "uhuru kwa papa".

"Kila sekunde, kila dakika wasiwasi wetu unaongezeka," Díaz, 26, alisema katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza.

"Mama yangu, mimi na kaka zangu tumekata tamaa, tunahangaika na hatuna maneno ya kuelezea kile tunachohisi, mateso haya yataisha tu tukiwa naye nyumbani.

"Naomba wamuachilie mara moja, wakiheshimu uadilifu wake na kukomesha kusubiri huku kwa maumivu. Kwa jina la upendo na huruma tunaomba wafikirie upya matendo yao na kuturuhusu kumpata tena."

Chanzo: Bbc