Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchawi wa makombe awindwa Misri

Herve Renard .jpeg Herve Renard

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Misri ipo katika hatua nzuri za kumnasa kocha, Herve Renard kwa ajili ya kuinoa timu yao Taifa ambayo imekuwa na msimu mbaya katika Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) mwaka huu huko Ivory Coast.

Uongozi wa chama cha mpira wa miguu Misri (EFA) unaripotiwa kuwa unaelekea kukaribia kufikia makubaliano na Renard ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa ya wanawake ya Misri ili aifundishe timu yao ya wanaume.

Uamuzi wa kumchukua Renard umekuja muda mfupi baada ya EFA kuvunja mkataba na kocha Rui Vitoria kufuatia timu hiyo kutolewa katika hatua ya 16 ya Afcon mwaka huu kwa mikwaju ya penalti 8-7 na DR Congo.

Herve amekuwa na historia ya mafanikio katika fainali za Afcon kwa kuziongoza timu mbili kutwaa ubingwa kwa nyakati tofauti, akifanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2012 akiwa na Zambia na kisha 2015 alipokuwa akiinoa Ivory Coast.

Mwaka 2022, Renard aliishtua dunia baada ya kuiongoza Saudi Arabia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Argentina katika mechi ya kwanza ya kundi lao katika fainali hizo zilizofanyika Qatar.

Chanzo: Mwanaspoti