Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi afunguka sababu za Tshabalala kutemwa Taifa Stars

Kapombe X Tshabalala Stars Mchambuzi afunguka sababu za Tshabalala kutemwa Taifa Stars

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Adel Amrouche mwenye asili ya Algeria ameacha kumjumuisha beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein kutokana na kiwango kizuri anachokionyesha beki Novatus Dismas aliyeko Ubelgiji.

Samwel Rashid amesema hayo kufuatia Amrouche kuita kikosi chake ambacho kitacheza na Algeria, Septemba 7, 2023 na kuwaacha baadhi ya nyota kama Tshabalala, Kapombe na Fei Toto.

"Upande wa kushoto kwenye eneo hilo ukijaribu kulinganisha Novatus pamoja na Zimbwe obviously utaona mwalimu amemwamini zaidi Novatus kwa sababu ya exposure ambayo Novatus anayo kwa sasa pamoja na Form ambayo Novatus anayo kwa sasa.

"Zimbwe anaweza akawa ni mchezaji mzuri lakini Form ya Novatus inaweza ikawa imeamua hatma ya Novatus kuwa favorite kwa Mwalimu mbele ya mchezaji kama Zimbwe," amesema Wakanda.

Baada ya kuwaacha nyota hao, maswali mengi yameibuka kwa nini kocha awaache wakati viwango vyao vinafahamika na wamekuwa msaada mkubwa kwa timu ya Taifa kwa muda mrefu kutokana na uzoefu wao kwenye mashindano makubwa.

Kwa upande wa Kapombe, ambaye anacheza kama beki wa kulia, Kocha Adel si mara ya kwanza kumuacha, amewahi kumtumia Dickson Job katika mchezo wa Uganda kule Mirsi na akapata matokeo mazuri huku Job akitoa assist ya bao kwenda kwa Simona Msuva.

Fei Toto bado hajawa fit kwa sababu amekaa nje ya uwanja kwa zaidi ya nusu msimu, hivyo anahitaji kufanya kazi kubwa ili kurejea kwenye ubora wake kwani nafasi yake wapo viungo wengi wanaoweza kucheza nafasi hiyo kama Mudathiri na wengine.

Katika mchezo huo, Taifa Stars inahitaji alama moja tu ili iweze kufuzu michuano ya AFCON 2023 wakati ALgeria tayari imeshafuzu michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: