Wakati Yanga wakionekana kufanya jitihada kubwa kuhakikisha wanavuka hatua inayofuata ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Mchambuzi wa Michezo kutoka Clouds FM, Farhan Kihamu anasema Yanga ina nafasi ndogo kupenye hatua ya Robo Fainali.
"Kama una ndoto ya kuingia makundi Klabu bingwa Afrika , ni mara chache sana unaweza ukaenda nje ya makundi ! Kama una ndoto ya kufika fainali maana yake utajiandaa kuwekeza kwa fainali ,mafanikio makubwa zaidi utakayoyapata itakuwa ni Nusu fainali au Robo fainali “
“Ukisema una ndoto ya kubeba taji ,maandalizi yako yanaweza yakakupa Nusu Fainali au Fainali “
“Yanga wao wanasema target yao ni makundi , unakubaliana nao kwa sababu ni timu ambayo inajitafuta kwenye mashindano ya Afrika , malengo yao waliyojiwekea hawana wanachodaiwa “
“Sioni kwenye lile kundi kama Al Ahly malengo yake ni kuishia makundi ,CR Belouizdad simuoni makundi , Medeama pia huwezi kuliona hilo , wakati mwingine unalaumu malengo waliyojiwekea"
Je unakubaliana na mchambuzi huyu? Tupe maoni yako