Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Viongozi wa Azam hawana uzoefu

Azam Kambi Uturuki Mchambuzi: Viongozi wa Azam hawana uzoefu

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa EATV na EA Radio, Albogast Myaluko anaamini kwamba kama Azam FC ingekuwa Morocco kwa pesa walizonazo wangekuwa wapo mbali sana kwenye soka la Afrika.

Albogast amesema hayo wakati akitoa maoni yake kufuatia Klabu ya Azam kutolewa kwenye michuani ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa na Bahir Dar Kenema FC kwa mikwaju ya penati.

"Tuwapongeze Azam Fc kwa sababu ndani ya miaka yao ya kuanzishwa wamefanikiwa kuchukua Ligi Kuu, wanakamata nafasi ya pili na wakati mwingine nafasi ya tatu, wameonyesha upinzani sahihi kwenye Ligi ya ndani.

"Licha ya uwekezaji wao mkubwa, hata Pyramids FC anapitia hicho hicho kwenye ligi ya anachokipitia Azam Fc kimataifa. Pyrmaids amefanikiwa kufika fainali ya CAF sababu ya nguvu ya taifa, aina ya wachezaji na urahisi wa kupata taarifa sahihi za michuano na huduma za michuano tofauti na Tanzania.

"Azam wangekuwa kwenye Taifa kama Morocco na pesa zao walizonazo ingekuwa rahisi kupata huduma nyingi za kimpira kuliko hapa kwetu. Kuna njia hata wao Azam tu imekuwa ngumu kuzipata kwa ndani. Ukienda Kimataifa, uzoefu wa viongozi wao namna ya kuyaenea mambo bado hawana uzoefu.

"Chukua viongozi wote Simba, Yanga, TFF jiulize imewachukua miaka mingapi kufuzu AFCON tangu mwaka 1979? Ni kitu ambacho kinakuja polepole, kwa hiyo waliopo nyuma ya Simba na Yanga watazidfi kufuata hii process ya kupiga hatua taratibu. Lakini kwa vile wana pesa tunataka waruke process ya soka,” amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live