Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Sioni faida timu kwenda Pre-Season nje ya nchi, ni ushamba

Simba Kambi Nje Mchambuzi: Sioni faida timu kwenda Pre-Season nje

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Vikosi vya Azam FC na Simba SC wakienda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kujiandaa na Ligi Kuu na Michuano ya CAF.

Azam tayari wapo nchini Tunisia huku Simba wakijiandaa kusafiri kesho Julai 12 kwenda nchini Uturuki.

Sasa mchambuzi wa Soka kutoka TV3, Alex Ngereza yeye amekuwa na maoni tofauti kwa Timu ziazokwenda kujiandaa na msimu mpya nje ya nchi.

Akizungumza amesema;

"Huenda hizi timu zetu hazielewi maana ya Pre- season, Timu za Ulaya zinafanya pre season kibiashara zaidi, wanakendwa pre season kwenye nchi ambazo zina Mashabiki wengi wa klabu hiyo lengo ni kwa ajili ya biashara na kushiriki makombe maalum waliohalikwa kwa muda huo"

"Lakini timu zetu zinakwenda nje ya nchi bila sababu yeyote ya msingi, Kwa mfano klabu ya Yanga msimu uliopita iliweka kambi ya maandalizi kigamboni na klabu ikabeba Ubingwa wa Ligi na ikafika fainali ya shirikisho."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live