Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Simba sasa ina watu!

Simba Kikosi Erd.jpeg Simba sasa ina watu!

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbele ya Mashabiki 60,000 mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, mbele ya Karia wa Karume, mbele ya Chalamila wa Dar Es Salaam! Danny Alves wa Matombo, Morogoro!

Shomari Kapombe alikuwa na mechi yake binafsi! First touch kama Mchizi Rick Ross wa Mayback kwenye yatch! Mtawaimba wote ila hizo verse zenu basi Kapombe leo ndio Chorus!

Kocha wangu Robertinho kutofanya mabadiliko ya Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kuna kitu amemaanisha, acha tujipe muda ila ana maana yake kubwa sana ambayo imenifikirisha sana, wamemaliza zote! Ina maana wataendelea kucheza sana.

Natamani kukiri kuwa Fabrice Ngoma ni Mtu sana, natamani kukubali Che Malone ni Kitasa sana, natamani kusema tuna Kipa imara sana ila napata ukakasi kwakuwa Dynamos hawakuwa ile timu ya kutupa ile mechi tuliyoitaka sana, walikuwa ‘unga’ sana.

Kuanzia kati mwa uwanja kwenda mbele Simba ni timu sana, ina watu sana hata akikosa Mtu flani huoni pengo sana, wanacheza kwa kupokezana! Onana anajua sana, Kramo dakika chache sana ila amepambana, Saido na Chama wanajuana sana!

Homeboy Aishi ugua pole na urejee haraka sana! Kesho kijiweni nitaanza ubishani wangu timu ipi ina ‘Mademu’ wakali sana maana Simba leo nimeona visu vya hatari sana, haki ya nani maua yalijaa sana?

Sijui kwanini ila najikuta bado nina hofu sana!We Zombie?

Na Farhan Kihamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live