Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Nani aliewaambia Albino anahitaji kuonewa huruma?

Biko X Manara Mchambuzi: Nani aliewaambia Albino anahitaji kuonewa huruma?

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati malalamiko yakiwa ni mengi baada ya jana katika kilele cha Tamasha la "Simba Day" kupandishwa Albino huku wengi wakisema kitendo hicho ni udhalilishaji.

Mchambuzi na mtaalamu wa Masoko Biko Scanda ameandika;

"Huyo pichani ni mwanadamu kamili, Mbunifu, ana ushawishi na ana nguvu ya kufanya jambo analotaka na wala hataki huruma ya mtu kufikia malengo yake. Ukiweka kila jambo pembeni huyu ndiye mwanadamu aliyeupa Hadhi Usemaji, ndiye alowapa kula hawa kina Ahmed Ally.

Haji Sunday Manara ni Albino, huyu ana macho, Mikono na Miguu na ana sauti ilojaa mamlaka pindi akipewa kipaza. Kwangu mimi huyu alipaswa kuwa mfano kwa vijana wote wenye UALBINO ya kwamba wao hawahitaji kukaa ndani kusubiri misaada na huruma bali wanapaswa kuingia vitani kupigania ugali na raha za Dunia.

Tukio la Jana la kumleta Muigizaji mwenye UALBINO jukwaani mie sikuona shida, kwangu mimi siwachukulii Albino kama watu wanaopaswa kuonewa Huruma ili waoneshe Vipawa vyao. Nani alimuonea Haji Huruma hadi kufika hapo..? Je, Haji anapotawala jukwaa kwa Ubora ni kutokana na Huruma na sio Uwezo…?

Kuna Tamthilia wanaigiza Albino, hakuna anayesema ni Udhalilishaji, kuna Yule Chiba wa Yamoto Band alikua anacheza na mguu mmoja hakuna aliyesema udhalilishaji na maigizo mengi yamefanywa jukwaani lakini hakuna anayepaza sauti. Iweje Kijana mwenye UALBINO anayetaka kufanya Maigizo jukwaani aonekane kadhalilishwa au kufanya aina fulani pekee ya sanaa..?

Muda wa kuamka, muda wa Kuamini Haji Manara yupo alipo sababu ya uwezo na sio Huruma ndio maana huwa ana uwezo wa kuifanya media imuongelee yeye tu. Buggati ni mfano, tuache kuwatia watoto wenye Albinism unyonge ya kwamba wao ni walemavu, hawawezi na wanastahili huruma na misaada au kwenda barabarani kuombaomba. Midhali wana viungo kamili basi waambiwe wakapambane na sio kuwajaza ujinga ya kwamba hawawezi

Zamani hata wanawake walikua wanaonekana watu wa kuonewa huruma lakini leo tuna Rais Mwanamke. Tutafika safari ya Albino nao wataonekana watu bila huruma wala kuwekwa makundi maalumu sababu wana AKILI, nguvu na utimamu. Kama Taasisi kubwa Yaani Yanga na Simba na hata Timu ya Taifa zimewahi kumuamini Albino basi hawa Sio Kundi maalumu wala sio WALEMAVU."

Je una maoni gani kwa andiko hili la Scanda? tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: