Baada ya mchezo dhidi ya KMC Juzi Jumatano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mahojiana na wanahabari Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alitamka maneno ambayo baadhi ya Wachambuzi wameziponda kauli za Kocha huyo.
Miongoni mwa wachambuzi hao ni Ahmad Mkunda, ambae ameandika;
"Juzi Nmesikia Kauli ya Kocha wa Yanga Nasridine Nabi Akitoa Malalamiko kwamba anachukizwa na performance ya baadhi ya Wachezaji ambao huwa hawapati nafasi kikosini waliocheza dhidi ya KMC.
Kocha Nabi anasema kuwa;
Kuna Wachezaji wameridhika hawataki kubadilika.. anadai kuwa kwenye timu kubwa kama Yanga Mchezaji atakayeamua kubadilika ndiye atakayepata nafasi. Huwezi kuwa mchezaji mkubwa kama hauna akili kubwa"
Kiukweli Hii kauli yake Sikubaliani nayo ni kama Tayar Ameanza Kulewa sifa Yani kuifunga TP Mazembe goli tatu kocha ameanza maringo.
Yani mchezaji msimu mzima hajacheza hata asilimia 30 au 40 ya games za ushindani. Halafu unataka performance kubwa.