Mtangazaji wa EATV na EA Radio, Albogast Myaluko amesema kuwa msimu huu wa soka 2023/24 utakuwa mbovu mno kutokana na mabadiliko makubwa ambayo yamefanywa na vilabu karibu vyote kwenye sajili za wachezaji wao walizofanya.
Pazia la msimu mpya limeshafunguliwa rasmi na leo michezo ya Ligi Kuu inaanza katika viwanja mbalimbali nchini.
"Mtazamo wangu nikitazama sajili zilizofanyika msimu huu tutakuwa na ligi mbovu sana kwenye nusu ya msimu. Ni kwa sababu timu zimefanya mabadiliko makubwa sana, timu nyingi zimefanya mabadiliko makubwa mno kuanzia benchi la ufundi.
"Kwa mfano chukulia Simba pale, amebaki Robertinho tu peke yake kutoka kwenye benchi la ufundi msimu uliopita, nenda Yanga kuna kocha mpya, njoo AzamFC utaona, nenda uwanjani kwa wachezaji utaona timu zote zimefanya mabadiliko makubwa sana" amesema Albogast Myaluko.