Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Haatim Abdul, amesema moja kati ya mafanikio waliyoyapata Simba kwenye usajili ni kufanikiwa kuwanasa wachezaji wenye wasifu wa juu katika nchi walizotoka.
Amesema, kitendo cha kumpata MVP wa Rwanda, MVP wa Cameroon pamoja na Luis Miquisson ambaye alifanya makubwa akiwa na Simba SC kabla ya kutimkia Al Ahly, kinatosha kabisa kuwavuta mashabiki wa timu hiyo.
“Ukiacha Simba Day, kurudi kwa Luis Jose Miquissone ni sherehe ya pili katika Kilele cha Wiki ya Simba Day, ukiangalia hata namna walivyowatambulisha hawa wachezaji, walianza na MVP Miquisson wakawa wamemweka mwishoni na walipomtambulisha sasa ni kama kuikamilisha sherehe, mtu huwezi kupanga kukosa Simba Day,” aliasma Haatim.