Mchambuzi Ahmad Mkunda ameishauri Serikali ya Tanzania Kwa Kushirikiana na CCM Kuuboresha Uwanja wa Lake Tanganyika Stadium Uliopo Mkoani Kigoma ili nao Uwe miongoni mwa viwanja vitakavyotumika Katika AFCON Mwaka 2027
"Tunahitaji Nchi kujipanga zaidi maana Tuna muda wa kufanya Maandalizi Hadi Mwaka 2027, Nishauri Michuano hii isichezwe Katika Uwanja Mmoja wa Mkapa tuboreshe viwanja vingine vya mikoani pia navyo vitumike Katika AFCON 2027"
"Nimeona Maboresho yameanza Katika Uwanja wa Mkapa pamoja na Uwanja wa Amani Uliopo Zanzibar, Tuboreshe pia viwanja vingine kama Lake Tanganyika Stadium,CCM Kirumba na Alli Hassan Mwinyi Nadhani hivi viwanja Vikifanyiwa marekebisho itakuwa njema sana Ili Michuano hii wasiifurahie watu wa Dar es salaam Pekee" Mchambuzi Ahmad mkunda