Fabrice Ngoma bado anaonekana kutokuwa na kasi uwanjani, Jambo ambalo linapelekea kuwa na faida upande mmoja tu, Simba ikiwa n mpira anauwezo wa kupiga pasi zenye faida kwa timu kuchezesha timu na kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma
Lakini timu inaposhambuliwa anashindwa kuwa na msaada katika nafasi yake kama kiungo wa chini, Hivyo inapelekea timu kufikiwa kirahisi katika eneo la kujilinda, Al Ahly kama wangekuwa makini katika kipindi cha kwanza wangefaidika na udhaifu huo na kupata kufunga mabao mengi
Kama kocha Robertinho anahitaji sana huduma yake katika kikosi cha kwanza anatakiwa kuanza kuwatumia viungo wote wa kati yani Mzamiru, Kanoute na Ngoma kwaajili ya kutengeza uwiano sawa katika kukaba,kusaidia kuzuia ngome ya ulinzi na kuichezesha timu