Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Hakuna Mkataba usiovunjika, kinachofanyika ni uhuni

Feisal Salum TFF 1 1140x640 Fei Toto

Sat, 6 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji ikitoa taarifa jana Mei kuhusiana na sakata la Kiungo wa Yanga Mzanzibari Feisal Salum " Fei Toto" kuwa wametupilia mbali shauri hilo na kudai kuwa mchezaji huyo bado ni mali halali ya Yanga.

Wadau mbalimbali wa Soka wameendelea kutoa maoni yao wengine wakitaka busara itumike baina ya pande hizo mbili.

Lakini kuna wale ambao wanaona TFF haijafanya maamuzi sahihi katika kutatua utata baina ya pande hizo mbili.

Miongoni mwao ni Mchambuzi wa Soka, Ahmed Mkuda anasema;

" Naungana na Fatma Karume kuwa Hakuna Mkataba wa Mchezaji Yeyote Katika Dunia Hii ambao hauvunijiki ila kama atavunja Mkataba kinyume na Utaratibu anatakiwa Kupigwa faini sio Kulazimishwa kurudi Katika Klabu yake wakati haitaki Tena hii sio Haki na huu ni Unyanyasaji Kwa Feisal Nashauri Waende CAS "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live