Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato wa mabadiliko Yanga wafikia hapa

Hersi Fa835 Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga.

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Yanga ulioanza mwaka 2021, unaelekea pazuri baada ya mambo kadhaa kukamilika.

Katika Mkutano Mkuu wa Klabu uliofanyika Juni 27, 2021, Wanachama wa Klabu ya Yanga waliafiki kwa pamoja mabadiliko ya katika na uendeshaji wa klabu.

Mchakato huo wa mabadiliko wenye awamu saba, tangu kuanza kwake hadi sasa awamu tatu tayari zimekamilika, huku zikisalia awamu nne kila kitu kukaa sawa.

Katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa ni mabadiliko ya katiba, zoezi hilo tayari limekamilika.

Awamu ya pili ilikuwa ni mabadiliko ya Uongozi wa Klabu kwa mujibu wa katiba mpya, ambapo tumepata Baraza la Wadhamini, Rais, Makamu wa Rais na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Timu ya Menejimenti.

Awamu ya tatu, zoezi la usajili wa Wanachama, Matawi na Mashabiki (Fans Engagement), tumefanikiwa kusajili kidigitali Wanachama hai 55,725, Mashabiki 728 na Matawi 10044.

Kinachofuata baada ya hapo ni awamu ya nne, hapa utafanyika Uthaminishaji wa Klabu, mchakato wa mzabuni wa kufanya kazi hii utatangazwa ndani ya wiki hizi tatu, tutaweza kujua thamani halisi ya Klabu ya Yanga pamoja na kujua mtaji wa kwenda nao kwenye kampuni.

Awamu ya tano ni kusajili Kampuni, itakayomilikiwa na Klabu ya Yanga kwa 99%+1% na baadae kuuza hisa zake mpaka 49%.

Awamu ya sita ni kuundwa kwa Bodi ya Wakurugenzi ambao watakuwa 9 kwa ujumla wao (5 kutoka Yanga + 4 kutoka kwa wawekezaji), Mwenyekiti wa Bodi kutoka upande wa Klabu ya Yanga ambao ndio wenye hisa nyingi (majority shareholder).

Mwisho kabisa katika awamu ya saba, utengezwaji wa mkataba maalum wa kukasimu madaraka ya uendeshaji wa mpira kutoka Kamati ya Utendaji kwenda kwenye Bodi ya Kampuni utafanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live