Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato wa mabadiliko Yanga bado kidogo tu

Mabadiliko Yanga X504 Mchakato wa mabadiliko Yanga bado kidogo tu

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amewatuliza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kuwaambia kwamba, mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu sio kwamba unachelewa, bali unakwenda kwa mpangilio maalum.

Mchakato huo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ulianza miaka miwili iliyopita ambapo ilikuwa ni makubaliano ya wanachama katika mkutano mkuu uliofanyika.

Akizungumzia jambo hiloo, Eng. Hersi amesema: “Watu wengi wanaweza kudhani tunachelewa kwenye ishu ya mfumo wa mabadiliko, lakini hatujachelewa, hivi karibuni tumeitangaza kamati inayosimamia kumalizia mchakato huo chini ya Alex Mgongolwa. Kamati hii inaanzia kwenye kupata thamani ya klabu na kwenda kwenye kufungua kampuni na kutafuta wawekezaji.

“Thamani ya Young Africans wakati mchakato unaanza miaka miwili iliyopita na sasa sio sawa, kwa sasa imepanda, tathmini ya sasa ikifanyika itatupa thamani kubwa kuliko ile ya miaka miwili iliyopita. Hii maana yake nini? Ina maana kwamba atakayenunua hisa za Yanga kwa sasa atainufaisha zaidi Yanga kuliko miaka miwili iliyopita.

“Kuhusu asilimia 51 za hisa kwa wanachama zinaleta faida gani kwa klabu, sisi kama uongozi tulikubaliana kwamba klabu hii ibaki kwa wanachama, kwa hiyo wawekezaji wakubwa ambao ni asilimia 51 ni wanachama, tungetaka kupata pesa, tungeiuza klabu asilimia 100 kwa mwekezaji, lakini tulichokifanya ni kuiacha klabu kwa wanachama.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live