Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbwana Samatta, Dhahabu tuliyoigomea kuipitisha kwenye moto

Goli La Samatta Laivusha Paok Europa.jpeg Mbwana Samatta, Dhahabu tuliyoigomea kuipitisha kwenye moto

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nafsi inaniuma kila nikikatisha vijiweni na kukutana na kauli za kuchukiza, ni kauli ambazo zimeshachoshwa na masikio yangu. Ni kauli za kutatanisha za chuki dhidi ya Mbwana Samata.

Vijiwe vya soka havijawahi kuipa thamani miguu ya samata. Jina la Mbwana Samata Kama ingelikuwa dhahabu, basi ni ile dhahabu ambayo wendawazimu wa soka wamegoma kuipitishwa kwenye moto ili ing'ae.

Minong'ono ya wengi juu ya jina la Samata imenifanya nipigwe na butwaa, mchezaji aliyeiheshimisha Tanzania ligi kuu England. Midomo ya mashabiki wa Genk hawakuchoka kuliimba jina lake. Kwanini Tanzania haimbwi, hapa ndio ubongo wangu uliukumbuka ule msemo wa wahenga" Nabii hakubaliki kwao".

Mechi dhidi ya Zambia website zote za soka zilionyesha ndiye mchezaji mwenye 'rates' kubwa uwanjani. Alikuwa na perfomance nzuri mno kuliko mchezaji yeyote lakini bado wendawazimu wa soka tulichagua tulichokiamini ety hakuwa bora uwanjani!, Inashangaza.

Wakati huu Tanzania ikijiandaa kukabiliana na Congo, ni mbwana samata ndiye anayesumbua kwenye vichwa vya mabeki wa Congo. Wakati timu pinzani zikiogopa jina na kiwango chake, huku kwetu hatujawahi kuliimba jina lake. '''Ama kweli nabii hakubaliki kwao''.

Kwangu mimi Mbwana Samata ndiye mchezaji bora wa muda wote Tanzania ninajua wachache ndio watasadiki kwa sababu tumechagua kutoipitisha dhahabu hii kwenye moto ili ing'ae

Chanzo: www.tanzaniaweb.live