Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbwa wakwamisha Uhamisho wa Fabinho kutua Al Ittihad

Fabinho Mbwa Mbwa wakwamisha Uhamisho wa Fabinho kutua Al Ittihad

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uhamisho wa nyota wa Liverpool, Fabinho kwenda Al-Ittihad uko hatarini kutokana na mbwa wake, kwa mujibu wa Daily Mail.

Imeelezwa Saudi Arabia imepiga marufuku kuingia na mbwa mwitu na kumpa wakati mgumu Fabinho ambaye anamiliki wanyama hao na anawapenda sana.

Hivi karibuni ripoti za kushtua zimedai kwamba uhamisho wa nyota huyo ulikuwa hatarini kwasababu mbwa wake hawaruhusiwi kuingia Saudi Arabia.

Habari hiyo iliyovujishwa Saudi Arabia na kusambaa kwenye ilieleza kuwa mbwa mwitu wamepigwa marufuku kutokana na kuwa kwenye orodha ya wanyama hatari na wakali.

Al-Ittihad iliwapa Liverpool ofa ya Pauni 40 milioni kwaajili ya nyota huyo wa kamataifa wa Brazil, 29, ambaye atakuwa akiingiza Pauni 425,000.

Hata hivyo, mchakato mzima umegonga mwamba na sasa Fabinho ataungana na wachezaji wenzake wa Liverpool baada ya kuachwa nje ya kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live