Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbuni yazinduka Championship

Ik Mbuni.jpeg Mbuni yazinduka Championship

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mechi kadhaa, timu ya Mbuni FC juzi iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Mashujaa, mechi ya Ligi ya Championship iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Ushindi huo umewawezesha kufikisha pointi 21 na kuendelea kupigania nafasi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kwa kuingia moja kwa moja kwenye nafasi mbili za juu, au kucheza mechi za mchujo kama inashika nafasi ya tatu au ya nne.

Mabao ya washindi yalifungwa na Erickson Kabegi, Michael Mgimwa akipachika bao la pili, huku la tatu likiwekwa kwenye kamba na Jonathan Masimba, kabla ya Hassan Timbe kukamilisha kwa kufunga la nne.

Matokeo ya mechi zingine za Championship iliyochezwa juzi yalikuwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wenyeji African Sports wakizabuliwa mabao 2-0 dhidi ya Kitayoce, Fountain Gate ikaichapa Pamba bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro, Copco ikalazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza dhidi ya Mbeya Kwanza, Transit Camp ikaidungua Ndanda bao 1-0, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, na Biashara United ikiwa Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya KenGold.

Kwa matokeo hayo, Kitayoce imekwea kileleni ikiwa na pointi 35, ikiiacha JKT Tanzania ikiwa na pointi zake 24 ambapo ilitarajiwa kucheza dhidi ya Gwambina ambayo ni kama imejitoa au imesusa kucheza michuano hiyo kwani haijafika uwanjani kwenye mechi kadhaa.

Wakati huo huo, straika wa kikongomani Ngoi wa Ngoi Fabrice wa Kitayosce na Mtanzania Deogratius Kulwa wa Pamba wanaongoza kwenye orodha ya wafumania nyavu wakiwa na mabao saba kila mmoja.

Wachezaji hao wanafuatiwa na wachezaji wawili wa JKT Tanzania waliofunga mabao sita kila mmoja ambao ni Edward Songo na Martin Kisi, huku Emmanuel Steven wa KenGold na Adam Uledi wa Ndanda, kila mmoja akiwa amepachika mabao matano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live